Mshukiwa wa mauaji ya mumewe akamatwa Nyamira

Jannet Moraa mwenye umri wa miaka 30, alifikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkuu wa Nyamira akidaiwa kumuua mumewe, Edwin Mosota.

Tom Mathinji
1 Min Read
Mshukiwa wa mauaji akamatwa Nyamira.

Maafisa wa Polisi wamemkamata mshukiwa anayedaiwa kumuua mumewe katika kaunti ya Nyamira.

Jannet Moraa mwenye umri wa miaka 30, alifikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkuu wa Nyamira akidaiwa kumuua mumewe, Edwin Mosota.

Kupitia ukurasa wa X, Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), ilisema mshukiwa huyo atazuiliwa kwa muda wa siku 10 katika kituo cha polisi cha Ekerenyo, akisubiri kukamilika kwa uchunguzi.

“Mshukiwa huyo atazuiliwa kwa siku kumi huku uchunguzi ukiendelea kubainisha chanzo cha kifo kwa mume wake,” Ilisema DCI.

Aidha, mshukiwa huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani Septemba 21, 2026, ili kutajwa kwa kesi hiyo.

TAGGED:
Share This Article