Tandabeleua la soka ya Kenya laendelea baada ya mkutano wa AGM kuahirishwa

Masaibu yanazidi kuongezeka katika soka ya Kenya kila kuchao huku kuanza kwa Ligi ya wanaume kukisalia katika hali ya ati ati ikiwa tayari imecheleweshwa kwa wiki mbili.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mkutano mkuu wa mwisho wa mwaka ulioratibiwa kufanyika Alhamisi Septemba 10 uliahirishwa kutokana na kukosa akidi ya wanachama wa baraza Kuu waliohitajika ili kuanza.

Hii ilisababishwa na kujiondoa kwa wanachama saba wakiongozwa na naibu Rais McDonald Mariga,wakipinga baadhi ya Agenda zilizokuwa zimeorodheshwa kwa kikao hicho.

Masaibu yanazidi kuongezeka katika soka ya Kenya kila kuchao huku kuanza kwa Ligi ya wanaume kukisalia katika hali ya ati ati ikiwa tayari imecheleweshwa kwa wiki mbili.

FKF ilitoa arifa kwa vlabu vyote vya ligi ya wanaume kuwa msimu mpya utang’oa nanga Septemba 19,lakini yaonekana hali si hali ndani ya shirikisho.

Bado hali ni ya vuta ni kuvute kuhusu usimamizi wa Ligi hiyo msimu wa mwaka 2026/2027.

TAGGED:
Share This Article