Rais Ruto afanya ziara rasmi South Rift

Kwenye ziara hiyo, kiongozi wa taifa anatarajiwa kukagua na kuzindua miradi kadhaa ya maendeleo katika kaunti za Bomet na Kericho.

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William Ruto aanza ziara rasmi katika eneo la South Rift.

Rais William Ruto leo Jumatano ameanza ziara rasmi ya siku nne katika eneo la South Rift.

Kwenye ziara hiyo, kiongozi wa taifa anatarajiwa kukagua na kuzindua miradi kadhaa ya maendeleo katika kaunti za Bomet na Kericho.

Miongoni mwa miradi ambayo anatarajiwa kukagua ni pamoja na ujenzi wa uwanja mdogo wa ndege wa Itembe, hospitali ya mama na mtoto ya Bomet na ujenzi wa barabara Bomet mjini.

Miradi mingine atakayokagua ni ujenzi wa uwanja wa Kapkatet na shule ya msingi ya Rungut huku akitarajiwa kuwahutubia wananchi katika maeneo tofauti ya South Rift.

Ziara hya South Rift inajiri baada ya ziara ya kufana katika kaunti ya Kajiado juma lililopita.

Rais Ruto amekuwa akitembelea maeneo mbalimbali nchini ama kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali yake au kuzindua mingine kwa manufaa ya raia.

Akiwa kwenye ziara hizo, ameelezea kuwa miradi hiyo ni ishara ya wazi ya kazi inayofanywa na serikali yake kwa manufaa ya raia.

Ameutaka upinzani kuelezea utakachowafanyia Wakenya ikiwa utashinda uchaguzi mkuu ujao badala ya kuwachosha na kaulimbiu za “Kasongo” na “Wantam.”

 

Share This Article