Mumewe Rais Samia Suluhu wa Tanzania afariki

Martin Mwanje
1 Min Read
Hafidh Ameir Hassan, marehemu mumewe Rais wa Tanzania Samia Suluhu

Mumeme Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania, Hafidh Ameir Hassan, amefariki.

Hafidh alifariki mapema leo Jumatatu wakati akitibiwa ugonjwa wa moyo.

Akitangaza kifo hicho, Makamu mpya wa Rais wa nchi hiyo Deogratius Ndejembi alisema Hafidh alifariki wakati akipokea matibabu katika hospitali ya kumbukumbu ya Emilio Mzena visiwani Zanzibar.

“Ndugu wananchi, kwa masikitiko makubwa, nawajulisha taarifa ya kifo cha Mhemimiwa Hafidh Ameir Hassan, mume wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kilichotokea leo, tarehe 7, Septemba 2026 majira ya saa mbili asubuhi katika hpsitali ya kumbukumbu ya Emilio Mzena Zanzibar alipokuw akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa moyo,” alitangaza Ndejembi.

Mipango ya mazishi inaendelea.

Share This Article