Uganda na Tanzania zatwaa ubingwa wa CECAFA kwa shule

Kennedy Okwi alipachika bao pekee na la ushindi kwa Uganda kunako dakika ya 39.

Dismas Otuke
1 Min Read

Uganda na Tanzania zimetwaa Kombe la CECAFA baina ya shule za ukanda wa Afrika Mashariki kwa wavulana na wasichana mtawalia katika mashindano yaliyokamilika nchini Rwanda.

Uganda ilinshinda taji ya wavulana baada ya kuwalemea wenyeji Rwanda bao moja kwa bila wakati Tanzania, ikiwatitiga Kenya magoli 3-0, katika fainali ya wasichana.

Kennedy Okwi alipachika bao pekee na la ushindi kwa Uganda kunako dakika ya 39.

Mashindano hayo yalishirikisha shule za ukanda wa Afrika mashariki na kati.

 

Share This Article