Wanariadha wa Kenya watajitosa uwanjani Jumamosi usiku katika siku ya pili na ya mwisho ya mashindano ya Diamond League mkondo wa Brussels,Ubelgiji.
Wakenya watashuka uwnjani wakinuai kupata ushindi na kuzoa donge non takriban shilingi milioni saba na ushei pamoja na tiketi ya kushiriki makala ya kwanza ya mashindano ya donge na tiketi ya kushiriki mashindano ya Ultimate .
Mshindi wa nishani ya shaba ya dunia Reynold Cheruiyot atakimbia mita 5,000 pamoja na Corenelius Kemboi na jacob Krop ,wakimenyana na Grant Fisher wa Marekani na Biniam Mehary miongoni mwa wengine huku fainali hiyo ikianza saa tatu na dakika 22.
Mshindi wa nishani ya fedha ya Dunia Dorcas Ewoi ndiye Mkenya pekee atakayeshiriki mita 1500, kufuatia kujiondoa kwa bingwa mara tatu wa Olimpiki Faith Kipyegon.
Baadaye saa nne na dakika 20 usiku itakuwa zamu ya bingwa wa Jumuiya ya Madola Edmund Serem, kuwania kitita katika mita 3,000 kuruka maji na viunzi pamoja na Simon Koech na Wilberforce Kones wakitoana jasho na Godana Gemenghu na Samuel Firehu wote kutoka Ethiopia na Soufiane El Bakkali wa Morocco.