Rais Ruto azindua miradi kadhaa ya maendeleo Kajiado

Aidha, Rais alisema ataharakisha mchakato wa kutoa hatimiliki za ardhi hiyo na pia kwa wakazi wengine wa Kajiado.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto amezindua miradi kadhaa katika kaunti ya Kajiado siku ya Jumamosi huku akiendelea kunadi sera za serikali ya UDA.

Ruto alifungua mradi wa unyunyuziaji mashamba maji wa Nguruman Block A, huku akitangaza azma ya serikali kuwekeza shilingi nusu bilioni kuupanua ili kuimarisha kilimo.

Aliongeza kuwa mradi huo wenye ukubwa wa ekari 2,000, utawafaa pakubwa wakazi wa kaunti hiyo na kaunti nyingine zilizo karibu.

Rais pia alitangaza kuwa serikali itarejesha asilimilia 90 ya ekari 240,000 ya ardhi iliyotwaliwa na utawala wa Wakoloni kwa njia isiyo halali.

Aidha, Rais alisema ataharakisha mchakato wa kutoa hatimiliki za ardhi hiyo na pia kwa wakazi wengine wa Kajiado.

Share This Article