Rais Ruto azindua miradi kadhaa ya maendeleo Kajiado

Pia amesema ataharakisha mchakato wa kutoa hatimiliki za ardhi hiyo na pia kwa wakazi wengine wa Kajiado.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto amezindua miradi kadhaa ya maendeleo katika kaunti ya Kajiado siku ya Jumamosi huku akiendelea kunadi sera za serikali ya UDA.

Ruto alifungua mradi wa unyunyuziaji mashamba maji wa Nguruman Block A, huku akitangaza azma ya serikali kuwekeza shilingi nusu bilioni kuupanua ili kuimarisha kilimo.

Aliongeza kuwa mradi huo wenye ukubwa wa ekari 2,000 utawafaa pakubwa wakazi wa kaunti hiyo na kaunti zingine zilizo karibu.

Rais pia alitangaza kuwa serikali itarejesha asilimilia 90 ya ekari 240,000 ya ardhi iliyotwaliwa na utawala wa Wakoloni kwa njia isiyo halali.

Aidha, amesema ataharakisha mchakato wa kutoa hatimiliki za ardhi hiyo na pia kwa wakazi wengine wa Kajiado.

Share This Article