Ghana yamrejesha Carlos Queiroz kuwa kocha mkuu wa Black Stars

Kocha huyo alikuwa ameteuliwa kuingoa Black Stars siku 72,kabla ya kuanza kwa fainali za Kombe la Dunia alipowaongoza hadi raundi ya 32.

Dismas Otuke
1 Min Read

Carlos Queiroz ameteuliwa tena kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ghana,almaarufu Black Stars ,ikiwa miezi miwili pekee tangu ajiuzulu kufuatia msururu wa matokeo mabovu katika fainali za Kombe la Dunia .

Chama cha soka nchini Ghana kilitangaza kumteua tena mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 73, kutoka Ureno huku mtihani wa kwanza ukiwa mechi za kufuzu kwa kombe la mataifa ya Afrika,AFCON mwaka ujao.

Kocha huyo alikuwa ameteuliwa kuingoa Black Stars siku 72,kabla ya kuanza kwa fainali za Kombe la Dunia alipowaongoza hadi raundi ya 32.

Ghana wameratibiwa kucheza na Ivory Coast katika mechi za nyumbani na ugenini hatua ya makundikati ya Septemba 21 na Oktoba 6 mtawalia, kufuzu kwa kombe la AFCON mwaka ujao .

Share This Article