Wapenzi wa muziki wa Rhumba wa asili ya DRC wanaomboleza kifo cha mwanamuziki Carlito Lassa, kilichotokea huko Cincinnati, Ohio, nchini Marekani Agosti 31 2026.
Lassa ambaye jina lake halisi ni Charles Ndombasi Lassa alifariki akiwa na umri wa miaka 65, kutokana na kile kinachotajwa kuwa mshtuko wa moyo.
Carlyto Lassa alianza safari yake ya muziki katika bendi ya Singa Mwambe, Les Bourgeois na Bisengo kabla ya kujiunga na bendi maarufu maarufu ya TP OK Jazz akamalizia na Choc Stars, ambako alijijengea jina kama mwimbaji na mtunzi wa nyimbo.
Wakati wa kifo chake, Lassa alikuwa ameokoka na kutoa maisha yake kwa Kristo na alikuwa akihudumu kama mchungaji na msanii wa nyimbo za injili chini ya jina la Pastor Charles Ndombasi.
Anaacha nyuma sauti yake ya kipekee ambayo bado inakumbukwa katika nyimbo kama Riana akiwa na Choc Stars, pamoja na Verre Casse, Maya, Affaire Kitikwala, Ekoti ya Nzube na Ousmane Bakoyoko akiwa na TP OK Jazz.