Kawempe Muslim Ladies FC ndio mabingwa wa kombe la CECAFA baina ya vlabu vya Afrika Mashariki baada ya kuwalemea mabingwa wa Kenya ,Police Bullets FC, bao moja bila jawabu katika muda wa ziada wa fainali iliyopigwa Jumanne katika uwnaja wa Kigali,nchini Rwanda.
Timu zote zilitoshana nguvu kwa kukosa kufungana bao ndani ya dakika 90 na kubidi dakika 30 za mazidadi kuchezwa ambapo nahodha Agnes Nabukenya alipachika goli la pekee la na ushindi kwa mabingwa hao wa ligi ya Uganda.
Ushindi huo unawawezesha Kawempe kuwakilisha ukanda huu kwenye mashindano ya Kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika .
Aidha,Kawempe walijivunia kushinda mechi zote katika mashindano ya mwaka huu,wakifunga mabao 13 na kufungwa moja.