Mipango ya mazishi ya Omukama yaendelea, Museveni kupokea mwili Alhamisi

Mwenda zake mfalme alifariki wiki jana akiwa na umri wa miaka 34 akipokea matibabu ughaibuni baada ya kuugua kwa muda.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mipango ya mazishi ya Mfalme wa Tooro (Omukama) Oyo Nyimba Kabambu Iguru wa nne, imeanza rasmi leo Jumanne ikiongozwa na serikali. 

Rais Yoweri Museveni anatarajiwa kuupokea mwili siku ya Alhamisi.

Kulingana na mipango hiyo, mwili huo utawasilishwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe mapema Alhamisi, kutokea Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta nchini Kenya.

Mwenda zake alifariki wiki jana akiwa na umri wa miaka 34, akipokea matibabu ughaibuni baada ya kuugua kwa muda.

Share This Article