Mfalme wa Norway Herald wa tano afariki akiwa na umri wa miaka 89

Kulingana na Kasri ya mji wa Oslo, Mfalme Herald alifariki mapema Ijumaa katika hospitali ya kitaifa ya Oslo.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mfalme Harald wa tano wa Norway ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 89, baada ya kupelekwa hospitalini wiki jana kwa matibabu.

Kulingana na Kasri ya mji wa Oslo, Mfalme Herald alifariki mapema Ijumaa katika hospitali ya kitaifa ya Oslo.

Bendera ya Kifalme ilipeperushwa nusu mlingoti punde baada ya kutangazwa kwa kifo chake.

Herald alikuwa Mfalme wa kwanza aliyezaliwa nchini Norway tangu karne ya 14 na  alirithiwa na mwanawe
Haakon.

Hadi kifo chake, Herald wa tano alikuwa mamlakani kwa miaka 35, na atakumbukwa kwa kukiuka itikadi za Kifalme alipooa mke raia.

Share This Article