Nchimbi amwandikia Suluhu barua, aelezea nia ya kujiuzulu

Endapo Rais Samia ataidhinisha barua hiyo, Dkt. Nchimbi atakuwa Makamu Rais wa kwanza kujiuzulu afisini.

Dismas Otuke
1 Min Read

Makamu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ametoa notisi ya kujiuzulu kuanzia tarehe 19 mwezi ujao.

Dkt Nchimbi amemwandikia Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan barua ya kujiuzulu kwake kuanzia Septemba 19 mwaka huu, ambayo itakuwa mwaka mmoja tangu ashike hatamu za wadhifa huo.

“Agosti 27 mwaka uliopita, nilimuahidi Rais Dkt. Samia Suluhu kuwa nitatekeleza majukumu yangu kwa uadilifu na uwezo wangu. Pia nilimhakikishia kuwa siku nitakayohisi kuwa siwezi kutekeleza kazi yangu jinsi nilivyoahidi, nitamtaarifu. Nimemjuza kuwa leo kuwa muda wangu wa kutimiza ahadi yangu umetimia, na ningependa kujiuzulu,” alisema Dkt. Nchimbi kupitia kwa waraka huo.

Makamu huyo wa Rais aidha amemshukuru Rais kwa kuwa na imani naye na pia kuwashukuru Watanzania kwa kumuunga mkono wakati wake akiwa afisini.

Endapo Rais Samia ataidhinisha barua hiyo, Nchimbi atakuwa Makamu Rais wa kwanza kujiuzulu afisini.

Share This Article