Mtangazaji mkongwe ambaye pia alikuwa Mkurugenzi wa hafla za Rais Sammy Lui, ameaga duania.
Lui ambaye aliongoza hafla za Rais, wakati wa utawala wa Rais Daniel Arap Moi, alifariki Alhamisi asubuhi, kulingana na mwa wake wa kiume Chris.
Mtangazaji huyo alikuwa sehemu ya kundi ambalo liliwaleta pamoja watangazaji wakongwe ambao awali walifanyakazi katika iliyokuwa Sauti ya Kenya (VOK) sasa ikijulikana kama Shirika la Utangazaji Nchini (KBC).
“Sammy Lui Wang’ondu, alifariki Alhamisi Oktoba 23,2025 asubuhi. Nimepokea simu kutoka kwa mwaka wake wa kiume,” ilisema ujumbe kutoka kwa kundi la watangazaji wakongwe.
Kundi hilo linalojulikana kama VOK/KBC Icons, lina takriban watangazaji 200 wa sasa na wa zamani wa shirika hilo la serikali.
Lui ambaye alifahamika sana kutokana na sauti ya kipekee na ufasaha wa lugha ya kiingereza, alikuwa miongoni mwa watangazaji waanzilishi wa kampuni ya KTN katika miaka ya 90.
