Shule kote nchini zinatarajiwa kufunguliwa kuanzia leo Jumatatu, Agosti 24 kwa muhula wa tatu na wa mwisho mwaka huu.
Muhula huo utashuhudia wanafunzi wakikalia mitihani ya kitaifa ya KPSEA, KJSEA, K.C.S.E, na pia ile ya vyuo vya mafunzo ya walimu.
Aidha, muhula huo utakuwa mfupi huku shule zikitarajiwa kufungwa Oktoba 23.
Vyuo vya kutoa mafunzo ya walimu pia vitafunguliwa leo Agosti 24 na kufungwa Novemba 6.
Wanafunzi wanarejea shuleni badaa ya likizo ya takriban majuma matatu.