Ruto amwomboleza Jaji Joseph Mutava Mbalu

Rais ametuma risala za rambi rambi kwa mjane na pia jamii yote ya marehemu.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto ameomboleza kifo cha jaji wa Mahakama Kuu Joseph Mutava Mbalu,aliyefariki Jumamosi baada ya kuugua.

Marehemu alikuwa mumewe Mbunge wa Kibwezi East Jessica Mbalu.

Rais ametuma risala za rambi rambi kwa mjane na pia jamii yote ya marehemu.

Alimataja marehemukuwa aliyetumikia Mahakama Kuu kwa uadilifu.

Mbalu alihudumu kama Jaji mwaka 2011 akihudumu katika Mahakama ya Milimani, kabla ya kuondolewa mwaka 2016.

Taafira kushu kifo cha marehemu Jaji zaarifu kuwa aliaga dunia Ijumaa baada ya kupatwa na matatizo ya kiafya aliporejea kutoka mazishini.

Alikimbizwa katika hospitali ya Makindu kaunti ya Makueni alipofariki akipokea matibabu.

‎Wengine waliomwomboleza marehemu jaji Mbalu ni kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka na Seneta wa zamani wa Machakos Johnson Muthama.

Share This Article