Kenya Power yasaini kandarasi za utendakazi na zaidi ya wafanyakazi 6,000

Hatua hii inajiri baada ya majadiliano ya zaidi ya miaka 20 kati ya KPLC na chama cha wafanyakazi hao (KETAWU).

Dismas Otuke
1 Min Read

Kampuni ya usambazaji umeme nchini (KPLC) imesaini kandarasi za utendakazi na zaidi ya wafanyakazi 6,000 katika hatua inayolenga kuboresha utoaji huduma na utendakazi.

Hatua hii inajiri baada ya majadiliano ya zaidi ya miaka 20 kati ya KPLC na chama cha wafanyakazi hao (KETAWU).

KPLC itakuwa kampuni ya kwanza ya kiserikali kusaini kandarasi za utendakazi na wafanyakazi walio katika miungano ya wafanyakazi kulinana na sheria za mwaka 2025, za mashirika inayotaka mashirika kuwapa wafanyakazi kandarasi za utendakazi.

Mchakato huo uliongozwa na tume ya kuratibu mishahara ua wafanyakazi wa umma nchini SRC.

TAGGED:
Share This Article