Waziri wa Elimu Julius Ogamba amesisitiza kuwa shule zote za msingi, sekondari na vyuo vya mafunzo ya walimu nchini zitafunguliwa kwa masomo ya muhula wa tatu ilivyoratibiwa, Agosti 24.
Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari, Waziri Ogamba amekanusha madai yaliyozagaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa tarehe ya kuanza kwa muhula wa tatu imesogezwa mbele.
Aidha, muhula wa tatu kwa shule za sekondari ya chini nchini utaanza Agosti 24 huku shule zikitarajiwa kufungwa Oktoba 23.
Vyuo vya kutoa mafunzo ya walimu pia vitafunguliwa ilivyopangwa Agosti 24 na kufunga Novemba 6.
Pia Waziri amekariri kuwa mitihani ya kitaifa itaandaliwa kama ilivyopangwa.
Waziri amewataka walimu, wanafunzi na wazazi kujiandaa kwa muhula wa tatu, akiwataka pia kufuata maagizo na maelekezo kutoka kwa wizara hiyo pekee.