Helikopta ya watalii imeripotiwa kuanguka karibu na Mlima Ololokwe katika kaunti ya Samburu.
Hatima ya waliokuwamo bado haijabainika.
Helikopta hiyo yenye makao yake katika eneo la Loisaba iliripotiwa kuwachukua watalii kutoka kambi ya Suiyan.
Timu ya uokozi inasemekana kuelekea eneo la ajali hiyo, ingawa maelezo ya kina kuhusu ajali hiyo bado hayajabainika.
Tutakupa maelezo zaidi punde tukipata taarifa.