Morocco yapitisha sheria ya wanyama wanaoranda ikijiandaa kwa Kombe la Dunia 2030

Sheria hiyo inapinga kuuawa kiholela kwa mbwa koko na wanyama wengine wanaorandaranda mitaani kama njia ya kupunguza idadi.

Dismas Otuke
1 Min Read

Morocco imepitisha sheria za  kudhibiti wanyama wanaozurura mitaani inapojiandaa kuwa mwenyeji wa kipute cha Kombe la Dunia mwaka 2030.

Sheria hiyo ilirasimishwa Agosti 10 na kuanza kutekelezwa Ijumaa iliyopita na inalenga kubadilisha jinsi mbwa koko wanavyoshughulikiwa nchini humo.

Wabunge 74 walipiga kura kuunga mkono sheria hiyo mpya nao wengine 21 wakakosa kupiga kura.

Sheria hiyo inapinga kuuawa kiholela kwa mbwa koko na wanyama wengine wanaorandaranda mitaani kama njia ya kupunguza idadi.

Mashirika ya kimataifa ya wanyama na vyombo vya habari vya kigeni vimekuwa vikishutumu jinsi wanyama wanaorandaranda wamekuwa wakidhulumiwa nchini humo.

Share This Article