Diamond ampokea Trey Songz Tanzania

Songz yuko Tanzania kwa ajili ya tamasha ya IMBEJU Sauti Moja, itakayofanyika kesho Ijumaa Agosti 14, 2026.

Marion Bosire
1 Min Read

Msanii nyota wa muziki nchini Tanzania Diamond Platnumz ameshiriki mapokezi ya mwanamuziki wa Marekani Trey Songz katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam usiku wa muamkia leo.

Songz yuko nchini Tanzania ambapo atakuwa mtumbuizaji mkuu katika tamasha ya IMBEJU Sauti Moja, itakayofanyika kesho Ijumaa Agosti 14, 2026 katika uwanja wa Posta wa Kijitonyama.

Diamond na Trey ni wanafahamiana kutoka awali hata kabla ya mapokezi hayo, ambapo waliwahi pia kuonekana wakiwa studio pamoja nchini Marekani.

Tamasha ya IMBEJU Sauti Moja, imeandaliwa na wakfu wa benki ya CRDB na linatumika kama uzinduzi rasmi wa awamu ya 7 ya mbio za Marathon za Kimataifa za CRDB zitakazofanyika Jumapili, Agosti 16.

Fedha zitakazochangishwa katika tamasha na mbio hizo zinatarajiwa kusaidia kuwezesha vijana kupitia mpango wa IMBEJU, huduma za afya kwa wajawazito walio katika hatari kubwa na upasuaji wa kuokoa maisha wa moyo kwa watoto.

Wasanii wakuu watakaotumbuiza ni pamoja na Trey Songz, BNXN kutoka Nigeria, Kabza De Small wa Afrika Kusini na wasanii wa Tanzania Mbosso na G Nako kati ya wengine.

Share This Article