Kenya ina uwezo wa kufikia kiwango cha mataifa yaliyostawi, asema Prof. Hino

Mtaalam huyo wa kiuchumi alihimiza Kenya kuharakisha ukuaji wa kiuchumi, kuimarisha sera zake za kifedha, kuongeza uwekezaji katika miundomsingi na kuthibiti deni la umma.

Tom Mathinji
1 Min Read
Prof Hiroyuki Hino. Mshauri wa maswala ya Uchumi.

Mshauri wa kimataifa wa maswala ya uchumi Prof Hiroyuki Hino, ameelezea matumaini yake kwamba Kenya ina uwezo mkubwa wa kuafikia mageuzi ya kiuchumi na kijamii.

Akizungumza leo Jumatano wakati wa kongamano la kitaifa kuhusu ruwaza ya mwaka 2060, Prof. Hino alitoa wito kwa taifa hili kuchukua hatua za kijasiri ili kuchochea ukuaji wa uchumi.

“Kwa walio na shaka, ningependa kusema kuwa Wakenya na kile kinachohitajika kufanikisha ukuaji usio wa kawaida,” alisema profesa huyo.

Prof. Hino  ambaye wakati mmoja alikuwa Mshauri Mkuu wa kitengo cha Afrika cha Shirika la Fedha Duniani (IMF), alisema ingawaje pato la jumla nchini Singapore ni dola elf 80 ikilinganishwa na pato la jumla la Kenya la dola elf mbili,taifa hili lina uweza wa kufikia viwango vya ustawi wa kimaendeleo na kiuchumi vinavyoshuhudiwa nchini Singapore.

Mtaalam huyo wa kiuchumi alihimiza Kenya kuharakisha ukuaji wa kiuchumi, kuimarisha sera zake za kifedha, kuongeza uwekezaji katika miundomsingi na kuthibiti deni la umma.

Share This Article