TID azika tofauti na waandaaji wa miaka 30 ya Bongo Fleva

Angependa kujiunga na wasanii wenza wakongwe wa Bongo Fleva jukwaani Dodoma.

Marion Bosire
2 Min Read

Mwanamuziki wa muda mrefu wa muziki wa Bongo Fleva nchini Tanzania Top In Dar, TID ameamua kuzika tofauti zilizokuwepo kati yake na waandaaji wa tamasha ya miaka 30 ya Bongo Fleva.

TID ambaye jina lake halisi ni Khalid Mohamed, anasema hatua yake imechochewa na ukweli kwamba angependa kujiunga na wasanii wenza wakongwe wa Bongo Fleva jukwaani Dodoma.

Akizungumza kwenye video iliyosambaa mitandaoni, TID alisema kwamba kwa sasa yeye anafahamika kama Top In Dodoma ndiposa hataki wenzake waje nyumbani naye akose kuungana nao.

Mwimbaji huyo alisema kwamba yeye mwenyewe amekuwa kwenye ulingo wa muziki kwa miaka 30 na hivyo sherehe hiyo ni muhimu kwake pia.

Msanii huyo alisosa kuhudhuria tamasha kuu ya miaka 30 ya Bongo Fleva jijini Dar es Salaam Juni 10, 2016 na awamu ya pili ya mkoani Mwanza hivi maajuzi Agosti 8, 2026.

TID amesema amefikia uamuzi huo kutokana na umuhimu wa kushirikiana na wasanii wenzake katika kuenzi na kuendeleza muziki wa BongoFleva, ambao yeye amekuwa sehemu yake kwa miaka mingi.

Tamasha hiyo ya kusherehekea miaka 30 ya Bongo Fleva sasa inaelekea Dodoma ambako itafanyika Agosti 22, 2026 katika bustani ya Chinangali.

Mkongwe wa Bongo Fleva Dudu Baya naye awali alikuwa amedhihirisha tofauti na waandalizi wa tamasha hiyo lakini baadaye waliafikia makubaliano na amehusika katika awamu mbili za mwanzo.

Share This Article