Serikali kukumbatia uvumbuzi kuimarisha utoshelevu wa chakula

Kulingana na Mudavadi, maonyesho hayo yalidhihirisha jinsi kilimo cha kisasa kinavyoongeza uzalishaji, kuboresha mapato ya wakulima, kubuni nafasi za ajira na kuimarisha utoshelevu wa chakula.

Tom Mathinji
1 Min Read
Serikali kukumbatia uvumbuzi ili kuimarsha utoshelevu wa chakula.

Serikali imeelezea umuhmu wa sekta ya kilimo kama nguzo kuu katika ukuaji wa uchumi wa Kenya, utoshelevu wa chakula na maendeleo katika maeneo ya mashinani.

Akizungumza kwenye maonyesho ya kilimo ya Kaimosi, eneo la Emgwen, kaunti ya Nandi, Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi alidokeza klmo kinasalia kuwa uti wa mgongo wa taifa hili, kwa kuwa kinapiga jeki mamilioni ya familia kote nchin.

Alisema maonyesho hayo ambayo yamewavutia wakulima 10,000, watafiti, wabuni sera, wanafunzi na wafanyabiashara, ulidhirsha jinsi uvumbuzi, teknoloja na uongezaji dhamani unaweza imarisha kilimo cha hapa nchini.

Kulingana na Mudavadi, maonyesho hayo yalidhihirisha jinsi kilimo cha kisasa kinavyoongeza uzalishaji, kuboresha mapato ya wakulima, kubuni nafasi za ajira na kuimarisha utoshelevu wa chakula.

Aliwapongeza waandalizi wa maonyesho hayo Shirika la Chakula na Kilmo (FAO) pamoja na washrika wengine kwa kuleta maarifa, teknoloja na fursa za soko karibu na wakulima.

Aidha, alisema kuwawezesha wakulima ni muhimu katika kukabiliana na umaskini na kuhakikisha ufanisi wa taifa hili.

Share This Article