Tamasha ya kusherehekea miaka 30 ya muziki wa Tanzania almaarufu Bongo Fleva inapelekwa mjini Mwanza wikendi hii.
Awamu ya kwanza ya tamasha hiyo ambayo pia ilikuwa kuu iliandaliwa Julai 10, 2026, katika eneo la Mlimani City jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Sasa waandaaji wamesema kuwa Msanii Dudu Baya au ukipenda ‘Mamba’ atakuwa msanii wa tatu kupanda jukwaani katika tamasha hiyo Jijini Mwanza wikendi hii, Agosti 8, 2026, katika ukumbi wa The Climax, ndani ya jumba la Rock City.
Hatua hiyo wanasema imechochewa na maombi ya mashabiki wengi wa Bongofleva wa Mwanza ambao wanataka Dudu Baya atumbuize mwanzo kwani Mwanza ni nyumbani kwao.
Imechochewa pia na ombi la mamake mzazi ambaye hajawahi kushuhudia mwanawe akitumbuiza jukwaani hivyo anahitaji kumuona kabla hajalala.
Mbali na Dudu Baya, Wasanii watakaotumbuiza ni pamoja na Lady Jaydee, H Baba, Prezzo, AY, Fid Q, Chege, Juma Nature, Temba, Jay Moe, Soggy Doggy, Jafary, Ferooz, Daz Baba, Moxie, Tunda Man na Madee.
Wengine ni KR, Mr Blue, Dully Sykes, Joslin, Kalapina, Domokaya, Luten Kalama, Q Chief, 20 Percent, Lord Eyez, Rado, Mwasiti, Stara Thomas, Keisha, King Crazy GK, Solid Ground, Matonya, Baraka Da Prince, Mabaga Fresh na Mwana FA.
Wasanii wa Kenya, Jua Cali na Nyota Ndogo walipata fursa ya kutumbuiza katika tamasha kuu.