Tanzania kuanza mchakato wa kurekebisha katiba

Samia aliahidi kuwa  ataendelea  kufanya mikutano kila baada ya miezi mitatu na viongozi wa  vyama vya upinzani.

Dismas Otuke
1 Min Read

Tanzania imetangaza azma ya kufufua marekebisho ya katiba, huku juhudi za maridhiano ya kitaifa zikiendelea.

Rais Samia  Suluhu Hassan, alisema haya siku ya Alhamisi alipokutana na viongozi  kutoka vyama vinane vya kisiasa.

Aliongeza kuwa mchakato wa maridhiano na uwiano kisiwani Zanzibar, unaendelea vyem huku ukikaribia kukamilika.

Samia aliahidi kuwa  ataendelea  kufanya mikutano kila baada ya miezi mitatu na viongozi wa  vyama vya upinzani.

Mkutano huo ulihudhuriwa na wenyeviti pamoja na manaibu wa vyama vya kisiasa.

Share This Article