Harambee Starlets watimuliwa WAFCON na Senegal

Kenya waliopoteza mabao manne kwa bila dhidi ya Morocco, katika mchuano wa kwanza watarejea uwanjani Agosti 3, dhidi ya Algeria katika mechi ya kuhitimisha ratiba tu.

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya Kenya ya soka ya wanawake imebanduliwa nje ya fainali za Kombe la mataifa ya Afrika (WAFCON) nchini Morocco, baada ya kupoteza mechi ya pili mtawalia ,walipolazwa bao moja kwa bila na Senegal, Alhamisi usiku .

Starlets chini ya uongozi wa Beldine Odemba, walijipata taabani baada ya kupachikwa bao kunako dakika ya 35 kupitia kwa Seynabou Mbengue,huku juhudi zote za kukomboa bao zikidumazwa na Senegal waliojihami hadi kipenga cha mwisho.

Kenya waliopoteza mabao moja manne  kwa bila dhidi ya Morocco, katika mchuano wa kwanza watarejea uwanjani Agosti 3, dhidi ya Algeria katika mechi ya kuhitimisha ratiba tu.

Kenya aidha,imepoteza nafasi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia mwaka ujao,ambapo timu nne bora zitaikatia tiketi ya kwenda Brazil.

Starlets walikuwa wanashiriki WAFCON mwaka huu kwa mara ya pili na ya kwanza tangu mwaka 2016.

Share This Article