Bingwa wa Olimpiki na Dunia Faith Cherotich alidhihirisha umahiri wake aliponyakua nishani ya dhahabu huku akivunja rekodi ya mita 3,000 kuruka maji na viunzi katika Michezo ya Jumuiya ya Madola Jumatano usiku mjini Glascow, Scotland.
Cheroticha aliparakasa masafa na kuzikamilisha kwa rekodi mpya ya dakika 9 sekunde 1 .76, akiinyakulia Kenya dhahabu ya pili katika makala ya 23 ya michezo hiyo inayondelea.
“Nilikimbia kwa mbinu yangu, sikuwa naangalia nyuma. Nilikuwa na lengo moja tu, kutwaa ubingwa,”alisema Cheriotich baada ya kuibuka kidedea.
Kwenye matokeo mengine ya Jumatano, bingwa wa Dunia katika mita 800 Lillian Odira alifuzu kwa fainali baada ya kuongoza nusu fainali ya kwanza kwa muda wa dakika 1 na sekunde 59.39.
Upande wa wanaume, Brian Komen alifuzu kujiunga na bingwa wa zamani wa Dunia Timothy Cheruiyot katika fainali ya maili moja, licha ya kumaliza wa nne katika nusu fainali.
Hata hivyo, mshindi wa zamani wa nishani ya shaba ya Dunia Reynold Cheruiyot alipatwa na pigo baada ya kukosa kumaliza mbio hizo.
Zablon Ekwam pia alijikatia tiketi kwa nusu fainali ya mita 200 kwa kuweka muda bora msimu huu wa sekunde 20.42.
Kenya ni ya 12 katika msimamo wa medali ikiwa na dhahahbu 2, fedha 2 na shaba 2.
Makala hayo ya 23 ya michezo hiyo inayoandaliwa kila baada ya miaka minne, yatakamilika Jumapili hii, Agosti 2.