Michezo ya 23 ya Jumuiya ya Madola kuanza leo mjini Glascow,Scotland

Kenya ilimaliza ya 13 katika makala ya mwaka 2022 mjini Birmingham,Uingereza kwa medali 6 za dhahabu fedha 5 na shaba 10.

Dismas Otuke
1 Min Read

Makala ya 23 ya Michezo ya Jumuiya ya Madola yataanza rasmi leo usiku mjini Glascow, Scotland, huku ikileta pamoja wanamichezo wapatao 3,000 kutoka mataifa 74.

Jumla ya fani 10 za michezo zitashirikishwa na itakamilika Agosti 2.

Kenya inawakilishwa na wanamichezo 68 watakaoshindana katika fani za riadha,mpira wa kikapu kwa wachezaji watatu kwa wanaume na wanawake,Judo,unyanyuaji uzani,masumbwi,Netiboli pamoja na michezo ya walemavu.

Kenya ilimaliza ya 13 katika makala ya mwaka 2022 mjini Birmingham,Uingereza kwa medali 6 za dhahabu fedha 5 na shaba 10.

Wakati uo huo ujumbe mwingine wa Kenya uliondoka nchini Jumatano usiku kuelekea Scotland kwa michezo hiyo.

Michezo hiyo hushirikisha mataifa yaliyotawaliwa na Waingereza.

Share This Article