EAC kuzindua Taasisi ya Utafiti wa Virusi ya Uganda

Kituo hicho kitakachozinduliwa jijini Entebe, kitafanikisha utafiti wa virusi, utoaji mafunzo maalumu ya maabara, usimamizi wa maradhi, utambuzi wa magonjwa, na utoaji wa maarifa kwa nchi wanachama wa EAC.

Tom Mathinji
1 Min Read
EAC kuzindua Taasisi ya Utafiti wa Virusi ya Uganda, Jijini Entebe.

Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), imesema itazindua rasmi Taasisi ya Utafiti wa Virusi ya Uganda (UVRI) siku ya Jumatano.

Kulingana na EAC, kituo hicho kitakachozinduliwa jijini Entebe, kitafanikisha utafiti wa virusi, utoaji mafunzo maalumu ya maabara, usimamizi wa maradhi, utambuzi wa magonjwa, na utoaji wa maarifa kwa nchi wanachama wa EAC.

Kwenye taarifa, Naibu Katibu Mkuu wa EAC anayeshughulikia sekta za Miundombinu, Uzalishaji, Jamii na Siasa Andrea Aguer Ariik Malueth alisema, hatua hiyo inaonyesha ahadi ya jumuiya hiyo ya kuimarisha usalama wa afya wa kikanda kupitia ushirikiano na kuwekeza mifumo ya maabara.

Aidha, kulingana na Jumuiya hiyo, mpango huo ni sehemu ya mradi wa mtandao wa maabara wa kikanda wa EAC na unawiana na juhudi za kuimarisha mifumo ya afya chini ya Mkakati wa Afya ya Pamoja.

Share This Article