Mwijaku amshauri Zuchu

Anamshauri Zuchu asonga mbele kulingana na tangazo alilotoa la ndoa yake na Diamond kufikia kikomo.

Marion Bosire
1 Min Read

Mwanamitandao maarufu nchini Tanzania Mwijaku, amempa ushauri mwanamuziki Zuchu, baada yake kutangaza mwisho wa ndoa yake na Diamond Platnumz.

Alichapisha video mitandaoni inayomwonyesha akiwa na mke wake huku akisema, “Moja ya siku ambazo ninasimama na Zuchu ni siku ya jana, amefanyiwa madharau makubwa sana.”

Kulingana na Mwijaku, katika hafla ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya Mamake Diamond, Zuchu alidharauliwa kwa vile hawara wa Diamond aliitwa na kuheshimishwa katika mkutano huo ambao Zuchu hakuhudhuria.

Mwijaku ambaye jina lake halisi ni Burton Mwemba, sasa anamshauri Zuchu kusonga mbele kulingana na tangazo alilotoa la ndoa yake na Diamond kufikia kikomo.

“Wewe ni wa thamani, mpumbavu akiamua kukufanyia upumbavu, sio vizuri kumrejeshea upumbavu, wewe kaa kimya, songa mbele. Wewe ni mkubwa hufai kuchezewa” alishauri Mwijaku.

Katika video hiyo Mwijaku anaonekana kuthibitisha tena taarifa zilizoenea za Zuchu kujifungua anaposema, “Najua sasa hivi uko kwenye wakati mgumu wakati wa kujifungua wakati wa malezi lakini mwanaume uliyejitoea kumheshimisha anakufanyia upumbavu wa hali ya juu”.

Ushauri huu wa Mwijaku kwa Zuchu unafichua sababu iliyomsukuma Zuchu kutangaza kwamba ameachana na Diamond Platnumz.

Share This Article