Zuchu atangaza mwisho wa ndoa na Diamond

Haya yanajiri saa chache baada ya Diamond kuthibitisha Zuchu ana ujauzito.

Marion Bosire
1 Min Read

Msanii wa muziki nchini Tanzania Zuchu ametangaza kwamba ndoa yake na mwanamuziki mwenza Diamond Platnumz imekatika, baada ya mwaka mmoja tu.

Kupitia Insta Stories msanii huyo aliandika, “Mimi na aliyekuwa mwenzangu sasa tumetengana na tuko katika harakati za talaka.”

Aliendelea kuelezea kwamba anatangaza hilo kwa hisia kali baada ya kuwa na Diamond Platnumz kwa jumla ya miaka sita ikiwa ni mahusiano pamoja na ndoa.

“Namtakia aliyekua mwenzangu Naseeb Abdul na Familia yake kila la kheri,” aliendela kusema Zuchu kwenye ujumbe wake akiongeza kwamba kwa sasa anaangazia kupona na kulinda afya yake na kazi zake.

“Rizki imeisha Albamdulillah tulijaribu lakini Allah ana mipango yake na sina budi kuikubali ndio ubinadamu ndio maisha,” alimalizia mrembo huyo.

Haya yanajiri saa chache tu baada yake kukosa kuhudhuria usiku wa kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mamake Diamond Platnumz.

Katika mahojiano na wanahabari kwenye hafla hiyo, Diamond aliyekuwa ameandamana na Baba Levo alithibitisha kwamba Zuchu ni mjamzito ndio maana alishindwa kuhudhuria hafla hiyo muhimu.

Hatua ya Diamond ya kuthibitisha ujauzito wa Zuchu ilifuta taarifa ya awali aliyoitoa Zuchu akikanusha habari za kuwa mjamzito na kujifungua kwa siri.

Mwanamitandao wa Tanzania Maimartha alikuwa ametangaza awali kwamba Zuchu tayari amejifungua mtoto wa kike.

Share This Article