Ufaransa yaitonesha tena Morocco na kufuzu kwa nusu fainali

Dakika sita baadaye, Mbappe alimdokolea pasi Ousman Dembele aliyewahakikishia Ufaransa ushindi ambapo watakuwa wajkicheza kwa nusu fainali ya tatu mtawalia.

Dismas Otuke
1 Min Read

Ufaransa ndiyo timu ya kwanza kujikatia tiketi ya nusu fainali ya Kombe la Dunia mwaka huu baada ya kuwalemea Morocco mabao 2-0 katika robo fainali ya Alhamisi usiku uwanjani Boston nchini Marekani.

The Blues walianza kipindi cha kwanza kwa makeke na pasi za kuonana na kuwalazimu Morocco kujihami zaidi huku pia kipa Yaccine Bonou akilazimika kupangua mikwaju kadhaa ikiwemo penalti ya Kyllian Mbappe.

Kipindi cha pili, Ufaransa waliongeza shinikizo na iliwachukua dakika 15 pekee kwa Mbappe kupachika goli ka uongozi akiunganisha pasi ya Desire Doue.

Dakika sita baadaye, Mbappe alimdokolea pasi Ousman Dembele aliyewahakikishia Ufaransa ushindi ambaopo watakuwa wajkicheza kwa nusu fainali ya tatu mtawalia.

Ufaransa watakutana na mshindi kati ya Uhispania na Ubelgiji katika nusu fainali wanayoshiriki kwa mara ya tatu mtawalia.

Kwa mara ya pili mtawalia, Ufaransa iliwabandua Morocco nje ya Kombe la Dunia baada ya kuwatimua katika  nusu fainali ya mwaka 2022.

 

Share This Article