Nani ataenda nyumbani leo Kombe la Dunia kati ya Messi na Salah?

Pata uhondo wote kupitia runinga ya taifa KBC Channel 1 kuanzia saa moja usiku.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa watetezi Argentina watashuka uwanjani Atlanta, Marekani kukabiliana na Misri kuanzia saa moja usiku katika mechi ya raundi ya 16 bora.

Argentina inayoongozwa na Lionel Messi, itamenyana na Pharaohs ya Misri kwa mara ya pili katika historia baada ya  wawakilishi hao wa Amerika Kusini kuwazabua Misri 2-0 katika mechi ya kirafiki mwaka 2008.

Argentina waliongoza kundi J kwa pointi 9 baada ya kuwashinda Algeria, Austria na Uzbekistan na hatimaye kuhitaji muda wa ziada ili kuwashinda Cape Verde 3-2 katika awamu ya 32 .

Misri walipata ushindi dhidi ya New Zealand na kwenda sare na Iran na Ubelgiji, wakimaliza nafasi ya pili kundini G.

Katika 32 bora, Misri waliilemea Australia 4-1 katika penalti kufuatia sare ya bao moja.

Mafarao watalenga kujiunga na Morocco kama mwakilishi wa pili wa Afrika katika raundi ya 16 huku Argentina wakiwinda ushindi ndani ya dakika 90 ili kuepuka kucheza muda wa ziada.

Mwisho wa siku ya leo, huenda Messi au Salah akayaaga mashindano ya Kombe la Dunia.

Pata uhondo wote kupitia runinga ya taifa KBC Channel 1 kuanzia saa moja usiku.

Share This Article