Ubelgiji yazima ndoto ya wenyeji Marekani, Kombe la Dunia

Mashetani wekundu wa Ubelgiji wameweka miadi dhidi ya Uhispania kwenye robo fainali Julai 10 uwanjani Los Angeles.

Dismas Otuke
1 Min Read

Ndoto ya Marekani kucheza robo fainali ya Kombe la Dunia nyumbani ilikatizwa ghafla bin vuu mapema Jumanne baada ya kuambulia kichapo cha magoli 4-1 kutoka kwa Ubelgiji katika raundi ya 16 ugani Seattle.

Charles De Ketelaere alipachika mawili kunako kipindi cha kwanza kabla ya Hans Vanaken na nguvu mpya Romelu Lukaku kuongeza moja kila mmoja katika kipindi cha pili katika ushindi huo maridhawa.

Wenyeji walipata bao la kufuta machozi la dakika ya 31 kupitia kwa Malik Tillman.

Ubelgiji wameweka miadi dhidi ya Uhispania kwenye robo fainali Julai 10 uwanjani Los Angeles.

Matokeo hayo yanamaanisha kuwa hakuna mwenyeji yeyote atakayecheza robo fainali  mwaka huu, baada  ya  Canada na Mexico pia kutupwa nje na  Morocco na Uingereza mtawalia.

Share This Article