Mwangangi ataka mgao wa fedha kwa kaunti kuongezwa

radiotaifa
1 Min Read
Francis Mwangangi - Naibu Gavana wa Machakos

Naibu Gavana kaunti ya Machakos Francis Mwangangi sasa anasema mgao wa fedha ambao umekua ukitengewa serikali za kaunti hautoshi kutekeleza majukumu mbalimbali yaliyowekwa chini ya usimamizi wa serikali hizo.

Mwangangi anaeleza kuwa serikali za kaunti ndizo zenye majukumu mengi yanayohusu kutoa huduma kwa mwananchi wa kawaida.

Mwa msingi huo, anatoa wito wa kuongezwa kwa bajeti ya serikali hizo.

Ametoa mfano na sekta ya afya, maji, kilimo na barabara za nyanjani anazosema zinasimamiwa na serikali za kaunti.

Kulingana naye, hii ishara bayana kuwa serikali za kaunti zinatekeleza majukumu mengi na hivyo kuna umuhimu wa kuzitengea fedha za kutosha kwenye bajeti ili kuziwezesha kutekeleza majukumu hayo inavyostahili.

Taarifa ya Jonathan Musau 

Share This Article