Ruto: Vijana 2,500 wamenufaika na mradi wa NYOTA Wajir

Tom Mathinji
1 Min Read
Vijana 2,500 wamenufaika na mpango wa NYOTA kaunti ya Wajir.

Takriban vijana 2,500 katika wadi zote 30 kwenye kaunti ya Wajir, wamenufaika na mradi wa kuwapiga jeki vijana kiuchumi wa NYOTA, kupitia kupokea fedha za kuanza biashara, mafunzo na ushauri.

Kwenye hotuba yake kwa taifa wakati wa kuadhimisha sherehe za 63 za Madaraka za mwaka huu katika kaunti ya Wajir, Rais William Ruto alisema zaidi ya vijana 7,200 katika kaunti za  Wajir, Garissa, na Mandera wamefaidika pakubwa na mpango huo.

“Tunawekeza katika vituo vya kidijitali vya Jitume, vituo vya ICT , mipango ya kutoa maarifa kupitia dijitali na miundombinu ya kidijitali, ili vijana katika kaunti ya Wajir wapate fursa ya ushindani na vijana wengine nchini Kenya na kote duniani,” alisema Rais Ruto.

Kiongozi wa taifa aliwahimiza vijana wa Wajir kwamba, mustakabali wao hautazingatia mazingira yao, lakini ni kupitia talanta, maarifa na kujitolea kwao.

“Lakini talanta na bidii hunawiri wakati fursa na miundombinu ni thabiti. Ndio maana tunawekeza kwa watu na pia katika misingi ya mabadiliko ya kiuchumi,” aliongeza Rais Ruto.

Share This Article