Mawaziri wapya wa Museveni kupigwa msasa leo bungeni

Baraza jipya la Mawaziri alilolitangaza Rais Museveni, linawajumuisha Mawaziri 32 na wengine 50 wa idara za serikali.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mawaziri wapya wa Rais Yoweri Museveni wa Uganda,wataanza kupigwa msasa na bunge lao Juni mosi kabla ya kula viapo.

Wabunge watathmini kila Waziri baina ya Jumatatu na Jumanne kabla ya ripoti ya kutolewa kuhusu ufaafu wao katika Wizara zao.

Mawaziri hao wanaojumuisha wa Baraza la awali na wengine wapya, wataidhinishwa bunge kabla ya kuapishwa kuanza kutekeleza majukumu yao rasmi.

Baraza jipya la Mawaziri alilolitangaza Rais Museveni, linawajumuisha Mawaziri 33 na wengine 50 wa idara za serikali.

Share This Article