Ghana wabanduliwa na Colombia Kombe la Dunia

Atlas Lions watalenga kufuzu kwa awamu ya 16 bora kwa mara ya pili mtawalia baada ya kucheza hadi nusu fainali mwaka 2022.

Dismas Otuke
1 Min Read

Black Stars ya Ghana walitemwa  nje ya fainali za Kombe la Dunia baada ya kuambulia kichapo cha bao moja kwa bila na Colombia, katika raundi ya 32, iliyochezwa mjini Kansas nchini Marekani mapema Jumamosi.

Jhon Arias’ alifunga bao pekee kwa Colombia katika dakika ya 14 na kujihami hadi kipenga cha mwisho wakifuzu kucheza na Uswizi katika raundi ya 16 Julai 7 mjini Vancouver.

Mechi za Raundi ya 16 zitaanza Jumamosi usiku ,waakilishi wa Afrika Morocco ,wakikabiliana na Canada katika uwanja wa Houston,Marekani.

Atlas Lions watalenga kufuzu kwa awamu ya 16 bora kwa mara ya pili mtawalia baada ya kucheza hadi nusu fainali mwaka 2022.

Share This Article