Uswizi imefuzu kwa raundi ya 16 bora ya Kombe la Dunia kwa mara ya nne mtawalia baada ya kuwacharanga Desert Foxes ya Algeria mabao mawili bila jawabu katika mechi ya raundi ya 32 iliyopigwa mapema Ijumaa mjini Vancouver, Canada.
Breel Embolo na Dan Ndoye, walipachika magoli ya mwanzoni mwa vipindi vya kwanza na vya pili mtawalia na kuwapa ushindi huo ndani ya dakika 90.
Algeria walikosa fursa ya kujiunga na Morocco katika hatua ya 16 ya Kombe la Dunia mwaka huu.
Uswizi watasalia Vancouver ambapo watachuana na mshindi wa mechi kati ya Ghana na Colombia.