Kenya na Italia kuimarisha ushirikiano kukabiliana na uhalifu

Nchi hizo zimesaini Barua ya Dhamira kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika kuzuia na kukabiliana na uhalifu.

Martin Mwanje
1 Min Read
Waziri wa Usalama wa Taifa wa Italia Matteo Piantedosi na mwenzake wa Kenya Kipchumba Murkomen wakati wa kutia saini Barua ya Dhamira

Kenya na Italia zimetia saini Barua ya Dhamira kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika kuzuia na kukabiliana na uhalifu wakati ushirikiano wa usalama kati ya nchi hizo mbili ukizidi kuongezeka. 

Barua hiyo ilisainiwa na Waziri wa Usalama wa Taifa Kipchumba Murkomen na mwenzake wa Italia Matteo Piantedosi aliyemtembelea afisini mwake.

Piantedosi anafanya ziara rasmi humu nchini.

Barua hiyo ya Dhamira inatoa mpangokazi wa kuhamasisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili na mamlaka za polisi za nchi hizo, ikiwa ni pamoja na uhalifu wa kupangwa wa kimataifa.

“Kenya inakaribisha mbinu iliyounganishwa inayotambua uhusiano thabiti kati ya maendeleo, usimamizi wa uhamiaji, na usalama,” alisema Murkomen wakati wa utiaji saini barua hiyo.

Chini ya makubaliano hayo, pande hizo mbili zitatenga vituo vya mawasiliano ili kuunga mkono mipango na shughuli za ushirikiano wa kimkakati katika ngazi za pande mbili na nyingi.

Share This Article