FIFA World Cup: Mexico wapiga delji hadi raundi ya 16

Mexico watarejea katika uwanja wa Mexico City kukabiliana na mshindi kati ya Uingereza na DR Congo Julai 5 katika raundi ya 16.

Dismas Otuke
1 Min Read

Wenyeji wenza wa Kombe la Dunia mwaka huu Mexico wameilaza Ecuador  magoli mawili bila jawabu katika mechi ya saba ya raundi ya 32 iliyoandaliwa mapema Jumatano ugani Mexico City.

Mchuano huo ulicheleweshwa kwa takriban saa moja kufuatia mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha.

Mexico almaafuru El Tri, walifunga kazi kunako kipindi cha kwanza kupitia kwa magoli ya Julian Quinones na Raul Jimenez huku kipindi cha pili kikiwa na ukame wa mabao.

Mlinzi wa Ecuador Pierro Hincaipie alipigwa kadi nyekundu kwa kufunga mdomo akimzungumzia mchezaji wa Mexico.

Mexico watarejea katika uwanja wa Mexico City kukabiliana na mshindi kati ya Uingereza na DR Congo Julai 5 katika raundi ya 16.

Share This Article