Halaand awaadhibu tembo wa Ivory Coast

Bao hilo lilitosha kuwapa Norway ushindi na kufuzu kwa raundi ya 16 ambapo watamenyana na mabingwa mara tano Brazil.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mshambulizi Erling Halaand alitikisa nyavu kunako dakika ya 86 na kuwapa Norway bao la ushindi dhidi ya Ivory Coast katika mechi ya tano raundi ya 32 ya Kombe la Dunia Jumanne usiku.

Mchuano huo uliosakatwa katika uwanja wa Dallas jimboni Texas, Marekani, ulishuhudia Tembo wa Ivory Coast wakimiliki mpira kwa kiwango kikubwa ila wakakosa kumakinika katika lango la wapinzani.

Ivory Coast waliokuwa wakicheza katika raundi ya mwondoano ya Kombe la Dunia  kwa mara ya kwanza,walijipata taabani kufuatia kosa lililofanywa na mabeki wake na kumpa fursa Antonio Nusa kupachika bao la ufunguzi dakika ya 39.

Amad Diallo aliwarejesha Ivory Coast mchezoni kwa goli la dakika ya 74, lakini pia mabeki wao wakazubaa na kumwacha Halaand bila ulinzi na akapokezwa pasi aliyoitumbukiza nyavuni dakika ya 86.

Bao hilo lilitosha kuwapa Norway ushindi na kufuzu kwa raundi ya 16 ambapo watamenyana na mabingwa mara tano Brazil.

Share This Article