Mlinda lango na nahodha wa timu ya taifa ya Ujerumani Manuel Neuer ,ametangaza kustaafu kutoka soka ya kimataifa siku moja tu baada ya mabingwa hao mara nne wa Dunia kutupwa nje ya fainali za za mwaka huu zinazoendelea.
Neuer amestaafu akiwa na umri wa miaka 40 alipangua mikwaju kadhaa ya Paraguay, katika awamu ya 32 , ya Kombe la Dunia Jumatatu usiku ikiwemo penati moja.
Kipa huyo ameichezea Ujerumani katika fainali tano za Kombe la Dunia na alikuwa katika kikosi kilichonyakua Kombe hilo mwaka 2014 nchini Brazil,ila tangu hapo wamekuwa wakibanduliwa mashindanoni mapema.
Neuer alikuwa miongoni mwa wachezaji weny umri mkubwa katika kipute cha Kombe la Dunia mwaka huu pamoja na mshambulizi wa Ureno Cristiano Ronaldo,aliye na umri wa miaka 41,kiungo wa Croatia Luka Modric , aliye na miaka 40,kipa wa Scotland Craig Gordon,aliye na miaka 43,na Edin Dzeko wa Bosnia-Herzegovina aliye na miaka 40.