FIFA World Cup 2026: Simba wa Atlas, Morocco waitema nje Uholanzi

Morocco watarejea nchini Marekani Jumapili hii dhidi ya Canada katika raundi ya 16 bora.

Dismas Otuke
1 Min Read

Atlas Lions ya Morocco imekuwa timu ya kwanza ya Afrika kufuzu kwa raundi ya 16 ya Kombe la Dunia baada ya kuwazidi maarifa Uholanzi kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya bao moja mapema Jumanne.

Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa sare tasa katika mechi hiyo ya uwanjani Monterrey nchini Mexico, timu zote zikibuni nafasi haba za kufunga magoli.

Licha ya kumiliki mpira kwa kipindi kirefu, Morocco walizubaa na kumruhusu nguvu Wout Weghorst kupiga shambulizi na kutoa pasi kwa Cody Gakpo aliyetikisa nyavu dakika ya 71.

Simba wa milima ya Atlas hawakufa moyo na waliendelea ksuhambulia na kumiliki mpira vyema na kosa la nahodha Virgil Van Dijk la kushindwa kuondosha pasi ya juu ya Chemsdine Talbi katika dakika ya 90 na kumpata Issa Diop aliyeunganisha mpira kwa kichwa na kuwapa goli la kusawazisha.

Matokeo hayo ya 1-1 yalidumu hadi dakika 120 na katika matuta, timu zote zilikosa kumakinika na hatimaye Morocco wakashinda 4-3 na kufuzu kwa raundi ya 16 kwa mara ya tatu katika historia.

Morocco watarejea nchini Marekani Jumapili hii dhidi ya Canada.

Share This Article