Mechi za makundi Kombe la Dunia kufikia tamati Jumamosi usiku

Uingereza na Panama watafungua ratiba ya kundi L, kuanzia saa sita usiku wa manane uwanjani New Jersey mjini New York,Marekani.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mechi za mwisho hatua ya makundi kuwania Kombe la Dunia zitapigwa Jumamosi usiku, huku ratiba kamili ya raundi ya 32 bora ikitarajiwa kubainika.

Uingereza na Panama watafungua ratiba ya kundi L, kuanzia saa sita usiku wa manane uwanjani New Jersey mjini New York,Marekani.

Three Lions ya Uingereza ni sharti wapate ushindi ili kuwa na uhakika wa kuongoza kundi hilo.

Ghana-Black Stars watakuwa Philadelphia dhidi ya Croatia wanaohitaji sare, ili kufuzu kwa raundi ya 32 bora.

Chui wa Congo watapimana nguvu na Uzbekistan katika kundi K,saa nane unusu ,DRC wakihitaji ushindi kwa kila hali ili kufuzu kwa hatua ya 32.

Colombia na Ureno watashikana mashati katika mechi nyingine ya kundi K, itakayochezwa sambamba kuanzia saa nane unusu usiku mshindi akimaliza kileleni.

Colombia wanaongoza kwa alama 6 ,mbili zaidi ya Ureno wanaokalia nafasi ya pili.

Saa kumi na moja alfajiri ngoma itaelekea kundi J ,mabingwa watetezi Argentina watakumbana na Jordan, ambayo tayari imetimuliwa mashindanoni katika uchanjaa wa Dallas nao Algeria wapimane ubabe na Austria.

Share This Article