Messi angali kuongoza ufungaji mabao Kombe la Dunia

Messi amepachika mabao 5 akifuatwa na Vinicius Junior wa Brazil, Kylian Mbappe wa Ufaransa na Erling Halaand wa Norway kwa magoli manne kila mmoja.

Dismas Otuke
1 Min Read

Nahodha na mshambulizi wa Argentina Lionel Messi angali kileleni pa jedwali la ufungaji mabao baada ya siku 15 za kindumbwendumbwe cha Kombe la Dunia kinachoendelea nchini Mexico, Canada na Marekani.

Messi amepachika mabao 5 akifuatwa na Vinicius Junior wa Brazil, Kylian Mbappe wa Ufaransa na Erling Halaand wa Norway kwa magoli manne kila mmoja.

Deniz Undav wa Ujerumani, Johan Manzambi wa Uswizi, Brian Brobbey wa Uholanzi, Matheus Cunha wa Brazil, Ismael Saibari kutoka Morocco na Jonathan David wa Canada wamepachika mabao 3 kila mmoja.

Jumla ya mechi 60 zimesakatwa katika Kombe la Dunia mwaka huu na magoli 177 kufungwa.

Mabao 12 yamekuwa ya kujifunga huku wachezaji 10 wakipokea kadi nyekundu, zikiwemo 8 za moja kwa moja.

Share This Article