Ufaransa yaikomoa Norway na kumaliza kileleni

Ousman Dembele alipiga magoli matatu (Hat trick) yote ndani ya kipindi cha kwanza dakika za 7,20 na 32, huku Thelo Aasgaard akifunga la kufutia machozi kwa Norway, na kipindi cha kwanza kumalizikia kwa uongozi wa The Blues wa 3-1.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa mara mbili wa Kombe la Dunia Ufaransa, walikuwa na kazi lele mama walipowatitiga Norway mabao 4-1 ,katika mechi ya mwisho ya kundi I,Ijumaa usiku uwanjani  Boston.

Ousman Dembele alipiga magoli matatu (Hat trick) yote ndani ya kipindi cha kwanza dakika za 7,20 na 32, huku Thelo Aasgaard akifunga la kufutia machozi kwa Norway, na kipindi cha kwanza kumalizikia kwa uongozi wa The Blues ,wa  3-1.

Kipindi cha pili Norway walirejea kwa matao ya juu ila wakapoteza penati baada ya kipa wa Ufaransa Mike Maignan, kupangua tobwe  lake Jorgen Larsen.

Ufaransa walijipatia bao la funga kazi dakika ya mwisho ya mazidadi kupitia kwa Desire Doue.

Wafaransa waliongoza kundi I kwa pointi 9,tatu mbele ya Norway huku Senegal iliyowalabua Iraq mabao 5-0, katika pambano jingine ikiwa ya tatu kwa alama 3.

Share This Article