Simba wa Teranga kutoka Senegal walikuwa na kazi rahisi walipowatofya Simba wa Mesopotamia kutoka Iraq magoli 5-0, katika mechi ya mwisho ya kundi I uwanjani Toronto,Ijumaa usiku.
Habib Diarra ,alifukua karamu ya magoli kwa Senegal kunako dakika ya 4,na kudumisha uongozi huo hadi mapumzikoni.
Hata hivyo ,kadi nyekundu yake Rebin Selaka katika dakika ya 13,iliwaponza Iraq huku wakizidiwa nguvu kunako kipindi cha pili.
Simba wa Teranga walijipatia la pili kupitia kwa Ismaila Sarr kunako dakika ya 56,kabla ya Pape Gueye, kuongeza mawili dakika 59 na 71 naye Ilman Ndiaye, aktiskisha wavu kwa goli la tano zikisalia dakika nane kipenga cha mwisho kipulizwe.
Ushindi huo umewakweza Senegal hadi nafasi ya tano katika uorodheshaji wa timu 8 bora zilizo katika nafasi za tatu.